Jumamosi, 15 Aprili 2017

Habari mbaya kwa wawekezaji waliopo na wanaotarajia kumiliki mabas... Jana tumeshuhudia kuwekwa kwa jiwe la msingi kufungua ujenzi wa train za umeme kutoka Dar mpaka Moro mradi utakao chukua muda wa miezi 30 sawa na miaka 2.5... Train hizo zinaweza kukupeleka Dar to Moro kwa saa 1:30 wakati mabasi yanachukua masaa 3:30 mpaka masaa 4:00 tofati n zaidi ya masaa 2:00... Train hizo zitakapo kamilika zinaweza kukimba kwa speed ya 160km/h wakati speed limit nyingi za barabarani ni 60km/h hichi n nini km sio kifo cha usafiri wa mabasi... Tujiulize je abiria wa kipindi hicho watachagua basi lenye kupigwa tochi, ulanguzi wa tiketi, ubovu,.. n.k au train za umeme zitazokua na uhakika wa safari tena bila kuchimba dawa wa kusimama kula? Na mm navyowafahamu wabongo kuna wakati pesa sio kitu mtu anaweza kulipa Tsh 650 akapanda Mwendokasi toka Kimara mpaka Ubungo ili awahi kuliko kupanda Eicher, Tata, n.k.. kwa gharama ya Tsh 400.. hvyo mradi wa train za umeme ukikamilika usishangae watu wakahama mabasi kwa wingi na wengine kuamua kuishi Moro kabisa kisa urahisi wa usafiri... Inavyosemekana miradi kama hii itaenda ruti za DAR-MORO-MZA, DAR-TANGA-MOSHI-ARS, na DAR-MORO-IRG-MBEYA kwa kufufua na kuboresha miundombinu tuliyoipotezea... Hii itaua kabisa biashara ya mabasi na malori pale itakapokamilika... Je wakati huo tutapost nn humu kama sio mabehewa na vichwa vyake na group kuitwa TANZANIA REGIONAL TRAINS...ambazo ni major ruti hapa nyumbani Tanzania... hii ni kwa nia njema tu na ss tuwe na maendeleo kama waliotutangulia... Kwa taarifa hii n vyema wawekezaji kuangalia watakua na nafas gani muda huo utakapofika... Shikamoo train za umemee

Maoni 1 :

  1. Mabus yatakuwepo pia ndipo revolution kubwa itakapoonekan mfano G7 1600DD au hata 1800 changamoto ni kwa wanaoanza sasa hiv na hao ruti ya Morogoro hivyo mabus yawe ya kisasa kwa starehe zaidi pia inategemea na nauli itakuwa kiasi gani

    JibuFuta