Ijumaa, 10 Februari 2017

Tanzania regional roads:part two

T2 au Trunk road 2 ni barabara kuu ya Tanzania inayoanzia Chalinze mkoa wa Pwani kupitia Segera, Korogwe , Same, Moshi na Arusha  hadi mpaka wa Namanga. Huko  inaendelea mpaka Nairobi kwa jina la A104. Barabara hii ina urefu wa takribani kilomita 650 kwa upande wa Tanzania.
Kwa upande wa mabasi barabara hii inafanikisha ruti nyingi ikiwa pamoja na zile maarufu za Dar - Moshi - Arusha, Dar - Nairobi, Dar - Karatu, Dar - Rombo na Dar - Tanga. Inatumika na mabasi zaidi ya 100 ya kampuni zaidi ya 40 kila siku.
T2 ndio barabara ya kwanza Tanzania kuwa na mabasi aina ya Marcopolo yaliyoletwa na kampuni ya Royal coach kwa ruti ya Dar - Moshi - Arusha. Na ndio barabara yenye mabasi mengi aina ya Marcopolo kwa sasa.
T2 pia ndio barabara ambayo ambayo ina hoteli nzuri zaidi na migahawa inayohudumia abiria kwa njia ya mabasi,malori na magari binafsi (huduma, vyakula vizuri na vinywaji)
Ukitumia barabara ya T2 utaweza kuona daraja maarufu la Wami, Mlima mrefu zaidi Africa (Kilimanjaro), Mlima Meru na  Milima ya Upare bila kusahau huduma ya mananasi na machungwa ya kutosha pale Chalinze, Segera na Korogwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni